Advertisement

ZILIZOSOMWA SANA

advertisement

Propellerads

Sunday, June 19, 2016

Tagged Under:

"Nimeipa Mombasa Awards siku saba" Asema Khalid produza,pata kujua kwanini..

By: Unknown On: 3:45:00 AM
  • Share This
  • To Whom it may concern,
    #MOMBASA_AWARDS

    kwa miaka mingi wasanii wa pwani wamekuwa wakibebwa kama magunia ilihali wenzao wa Nairobi au Bongo wakibebwa kama mayai.Tuzo nyingi zilizopita zimekuwa na tabia ya kuweka wasanii kwa list zao bila taarifa, ilihali mshindi ashajulikana. Wasanii hao hao ndio watapiga promo awards hizo kila mahali mpaka mashabiki wao waamue ku support event hiyo. Lakini haya yote huwa hayana manufaa kwani hata show wakiperform usiku huo hata shilingi hawapati, wala hakuna special recognition yoyote.

    Najua huwa mwaandika proposals kwa makampuni kufadhili Tuzo zenu, lakini manufaa kwa wasanii wa pwani hakuna. Mtalipia ndege na hoteli wasanii wa Bongo na Nairobi, muwa treat kama VIPs na wenzao wa mombasa hamuwashughulikii. Hii ni wazi kuwa mmajifanyia Tuzo hizi kwa manufaa yenu wenyewe.

    Ili kukomesha tabia hii nimeamua kuwapa #MOMBASA_AWARDS siku saba kurekebisha swala hili kwani hata nyinyi mumefuata mkumbo huo. Kwanza mumeweka majina ya wasanii bila kuwataarifu na kuanza marketing ya awards zenu. Hicho ni kinyume cha sheria za Kenya. Msanii anang'ang'ana sana kufika pale alipo. Haumufanyii favor yoyote kwa kumu nominate. Hilo ni jasho lake na mnafaa kuliheshimu.

    Ili kukomesha tabia hii ni rahisi, wasanii wote waliowekwa kwenye list bila taarifa wataandikisha taarifa kwa lawyer wangu wakilalamika kutumika kwa majina yao kibiashara bila taarifa na maelewano. Na kila msanii atadai kulipwa kwa kutumika vibaya. Gharama za lawyer na mahakama nitazigharamia ilimradi hii tabia ikome. Na kabla kesi kuanza nitaomba mahakama isitishe Tuzo hizi na nyengine za kipuzi kama hizi indefinitely.

    Siku saba mnazo kuitisha mkutano Kwanza, kujijulisha nyinyi ni akina nani. Pili, mnamalengo gani na wasanii na Tuzo zenu. Tatu, wasanii watafaidika kivipi kwenye Tuzo hizo na baada ya Tuzo hizo. Na kwa nini mkaweka majina ya wasanii bila taarifa yao ambacho hicho ni kitendo cha kihuni. Na mumetumia criteria gani kuchagua wasanii, manake nimeona mumejiwekea tu wasanii kwenye list bila ujuzi, hekima na mwongozo dhabiti.

    Wacheni niwakumbushe tena, hamumufanyii favor msanii yoyote kwa kumu nominate kwa hizo Tuzo zenu kwani ni jasho Lake na haki yake.Mko na siku saba kurekebisha hili, Lau sivyo tukutane mahakamani....

    0 comments:

    Post a Comment